1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luanda. Shirika la Afya duniani WHO, latoa wito wa kupambana na virusi vya Marburg nchini Angola

9 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFP3

.

Shirika la afya la umoja wa mataifa WHO, limetoa wito wa kuongeza juhudi za kupambana na kuenea kwa virusi hatari vya ugonjwa wa Marburg nchini Angola. Ugonjwa huo umekwisha ua zaidi ya watu 180 hasa katika eneo la kaskazini ya nchi hiyo. WHO imeripoti kutokea vifo vingi kuliko kawaida miongoni mwa watu 205 waliopatikana na virusi vya ugonjwa huo tangu mwezi Oktoba mwaka jana , hasa katika eneo la mji ulioko kaskazini mwa Angola wa Uige. Ugonjwa huo umewakumba zaidi watoto chini ya umri wa miaka mitano. WHO imetaka kuwepo na juhudi za kuendelea ili kuudhibiti ugonjwa huo, kwa upande wa jumuiya ya kimataifa pamoja na viongozio nchini Angola, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27 vimeleta uharibifu mkubwa katika mfumo wa huduma ya afya.