LOS ANGELES.mioto bado yawaka California
25 Oktoba 2007Matangazo
Watu zaidi ya nusu milioni wametakiwa wazihame nyumba zao ili kuepuka mioto inayoendelea kuwaka katika sehemu kadhaa za jimbo la California nchini Marekani.
Gavana wa jimbo hilo amearifu kwamba watu watatu wamekufa . Watu wengine 40 wamejeruhiwa na nyumba 1500 zimeungua.
Rais Bush anaetarajiwa kuwasili California leo ili kuona kiwango cha madhara amelitangaza jimbo hilo kuwa la maafa.