1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lissu kuishitaki serikali ya Tanzania kimataifa

25 Septemba 2024

Makamu Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania bara, Chadema Tundu Lissu amesema ataishitaki serikali ngazi ya kimataifa kuhusiana na shambulio dhidi yake.

https://p.dw.com/p/4l4jy
Tansania Wahlen | Opposition Tundu Lissu
Picha: AFP

Lissu ameyaibua haya baada ya Gazeti la The Guardian la Uingereza kusema kampuni ya mawasiliano ya Tigo nchini humo, ilitoa mawasiliano yake ya simu kwa serikali yaliyofanya mienendo yake kufuatiliwa kwa karibu.

Akizungumza na waandishi habari mjini Dar es Salaam, Lissu amesema ataishitaki kampuni hiyo katika ngazi za kimataifa na kushinikiza itaje majina ya watu wa serikali waliotaka kupewa taarifa zake.Tundu Lissu na harakati za "mwanzo mpya" Tanzania

"Nani, nani, aliyefanya hayo, kwa ushahidi, tunataka majina, tunataka ukweli wote kutoka kwa serikali na kutoka kwa tigo, tusipoupata kwa serikali, tutaupata kwa tigo."

Katika Ushahidi uliotolewa kwa mujibu wa gazeti hilo, kampuni hiyo ya simu iliajiri aliyekuwa mfanyakazi wa jeshi la polisi, London Metropolitan Police, Michael Clifford, kama mchunguzi wa ndani.

Tundu Lissu: Siwezi kusema ninao uhakika wa usalama wangu

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Clifford alisikia katika kikao kuwa serikali ya Tanzania ilifuatilia mienendo ya Lissu, kwa kutumia simu yake.

Kesi inayoendelea London, kimsingi ni kesi ya ajira, iliyofunguliwa na Clifford akiishtaki kampuni hiyo ya simu kwa kumuachisha kazi baada ya kuhoji kuhusu mienendo ya kampuni hiyo ya simu, kufuatilia taarifa za wateja, akiwamo Lissu.

Lissu, anasema yanayoendelea Uingereza katika kesi hiyo ni sawa na nahau isemayo; Mungu si Athuman na kusema kuwa hakutegemea kama taarifa hizo zingeibuliwa wakati huu.

"Magufuli amekufa hawezi kutuambia ukweli, mrithi wake ambaye ni Samia Suluhu Hassan atupe majibu haya, atuambie."

Polisi Tanzania wamkamata Freeman Mbowe

Akiwa katika mkutano huo na wanahabari, Lissu  amesema, amenusurika kifo lakini shambulio lile limemsababishia kufanyiwa upasuaji mara 25 na serikali ya Tanzania haijamlipa.Viongozi wakuu wa Chadema watofautiana

Hata hivyo juhudi za kuupata uongozi wa kampuni mama ya Tigo, Millicom hazikufua dafu, hadi tunakwenda mitamboni.

Septemba 17, Lissuambaye pia ni mwanasheria na amewahi kuwa mnajimu mkuu wa kambi ya upinzani Tanzania, alishambuliwa kwa risasi akiwa maeneo ya Area D, Dodoma,

Baadaye, alisafirishwa kwa ndege hadi katika Hospitali ya Nairobi Kenya ambako alipokea matibabu kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu maalumu.