Wakazi wa kijiji cha Itungi, kilichopo katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa katika mkutano ambao unaendeshwa na kikundi cha kina mama cha IMCHA ambacho kinatoa elimu kwa wakazi wa kijiji hicho kuhusiana na afya ya uzazi na mtoto ambayo inaelezwa kuwa ni changamoto katika kijiji hicho na vinginevyo vya mkoa wa Iringa uliopo nyanda za juu kusini mwa Tanzania.