1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kesi dhidi ya wanachama wa kundi la waasi wa M23 yaanza

Josephat Charo
24 Julai 2024

Kesi ya watu 24 wanaotuhumiwa kuwa sehemu ya kundi la M23 imeanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kiasi miaka miwili na nusu tangu waasi hao walipoyateka maeneo makubwa ya eneo la mashariki la nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4igqG
DR Kongo | M23
Waasi wa M23Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Kesi ya watu 24 wanaotuhumiwa kuwa sehemu ya kundi la M23 imeanza leo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kiasi miaka miwili na nusu tangu waasi wa kundi hilo walipoyateka maeneo makubwa ya eneo la mashariki la nchi hiyo.

Soma: Mahakama ya Kijeshi nchini DRC yawahukumu kifo askari 22

Ni washukiwa watano tu ndio waliokuwepo wakati kesi hiyo ilipoanza katika mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa. Mshukiwa mkuu, mwenyekiti wa zamani wa tume ya uchaguzi, Corneile Nangaa kwa sasa bado anasakwa.

Nangaa alitangaza kuunda vuguvugu jipya la kisasa na kijeshi, Alliance Fleuve Congo, AFC, muungano wa makundi ya waasi likiwemo kundi la 23. Wizara ya sheria ya Congo ilitangaza siku ya Jumatatu kufunguliwa kwa kesi dhidi ya Nangaa na washirika wake.