Tume ya Kusimamia Mipaka na Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imeidhinisha sahihi milioni 1.2 zilizowasilishwa na chama cha Thirdway Alliance kwa lengo la kuyafanyia katiba marekebisho. Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema kuwa tume yake imetimiza matakwa yote yanayohitajika. Sikiliza taarifa ya Shisia Wasilwa.