1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas na Iran wakosoa hotuba ya Netanyahu Marekani

25 Julai 2024

Kundi la wanamgambo wa Hamas pamoja na wizara ya mambo ya nje ya Iran wamekosoa vikali hotuba ya Waziri wa Israel Benjamin Netanyahu mbele ya Bunge la Marekani.

https://p.dw.com/p/4ijhu
USA Washington 2024 | Netanjahu vor Rede vor US-Kongres
Picha: Kent Nishimura/Getty Images

Hamas jana jioni walimshutumu Netanyahu kwa kuudanganya umma kuhusiana na juhudi za kufikia makubaliano ya kuachiliwa mateka.

Taarifa ya Hamas imesema matamshi ya Netanyahu kuhusiana na kuachiliwa mateka ni uongo, inayopotosha maoni ya umma wa Israel, Marekani na kimataifa, huku wakimshutumu kwa kuzuia juhudi zote zinazolenga kumaliza vita na kufikia makubaliano hayo, licha ya juhudi za upatanishi zinazoendelezwa na Misri na Qatar.

Aidha, mapema leo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran Nasser Kanani alilikosoa vikali bunge la Marekani kwa kumkaribisha na kumshangilia Netanyahu, baada ya miezi tisa ya kile alichokiita mauaji ya halaiki.