Hali Visiwani Komoro
26 Machi 2008Matangazo
Majeshi hayo ya Komoro na pia yakiwemo kutoka Tanzania na Sudan, yameidhibiti hali ya mambo katika Anjouan, hivyo kutimiza ile ahadi alioitoa Rais Abdullah Sambi wa Komoro kwamba uasi uliofanywa huko Anjouan utamalizika karibuni.
Othman Miraji, alizungumza kwa simu na Salim Himid, waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Visiwa vya Komoro, na kumuuliza sasa Visiwa vya Komoro vinaelekea wapi?