Gaddafi aripotiwa kuuawa kwenye uwanja wa mapambano
20 Oktoba 2011Matangazo
Machache unayopaswa kujuwa kuhusu Gaddafi:
· Jina lake kamili ni Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi, alizaliwa tarehe 7 Juni 1942, katika mji wa Sirte, kaskazini magharibi ya Libya
· Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969 na kuondoshwa madarakani na waasi walioungwa mkono na Jumuiya ya Kujihami ya NATO mwaka 2011
· Utawala wake wa miaka 41 unatajwa kuwa wa nne kwa urefu kwa utawala usiokuwa wa kifalme. Alijiita Kaka Kiongozi, Mlinzi wa Mapinduzi na Mfalme wa Wafalme
· Kituo cha Televisheni cha Al-Jazeera kimeripoti kuwa Gaddafi ameuawa tarehe 20 Oktoba 2011 baada ya kukamatwa kutokana na mapigano kati ya walinzi wake na wapiganaji wa vikosi vya Baraza la Mpito linaloongoza sasa Libya