Umesikia kuhusu Filamu ya Black Panther? Filamu hiyo ambayo imepata umaarufu mkubwa baada ya kuzinduliwa duniani ikiwashirikisha waigizaji wote weusi, imegeuka kuwa maonyesho ya mitindo. Inaonyesha aina mbalimbali ya mavazi yanayopatikana kote barani Afrika. Mitindo kutoka makundi tofauti imezingatiwa waziwazi kwenye filamu hiyo. Msikilize Bruce Amani katika makala ya Vijana MchakaMchaka.