1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dissanayake ashinda uchaguzi wa urais nchini Sri Lanka

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Tume ya uchaguzi nchini Sri Lanka imemtangaza rasmi kiongozi anayeegemea siasa za kijamaa Anura Kumara Dissanayaka kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kumwangusha rais Ranil Wickremesinghe aliyemaliza muda wake.

https://p.dw.com/p/4kx2b
Mgombea wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake
Mwanasiasa wa NPP Anura Kumara DissanayakaPicha: Eranga Jayawardena/AP Photo/picture alliance

Tume ya uchaguzi nchini Sri Lanka imemtangaza rasmi kiongozi anayeegemea siasa za kijamaa Anura Kumara Dissanayake kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais na kumwangusha rais Ranil Wickremesinghe aliyemaliza muda wake. Taarifa ya Tume ya uchaguzi iliyochapishwa katika tovuti yake, imeonyesha kuwa Dissanayake mwenye umri wa miaka 55, alishinda kiti cha urais kwa asilimia 42.31 ya kura katika uchaguzi wa Jumamosi.Raia wa Sri Lanka wapiga kura ya kumchagua rais

Mwanasiasa huyo amembwaga kiongozi wa upinzani Sajith Premadasa aliyeshika nafasi ya pili na Wickremesinghe akimaliza katika nafasi ya tatu kwa mbali. Dissanayake anatarajiwa kuapishwa kesho Jumatatu. Kinyang'anyiro hicho kililazimika kuingia katika duru ya pili ya kuhesabu kurakati ya Dissanayake na Premadasa baada ya duru ya kwanza kumalizika bila mshindi kwa asilimia 50.