1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR:Kitisho cha njaa chaendelea Niger

17 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEaH

Watoto bado wanaendelea kukabiliwa na kitisho cha kufa njaa nchini Niger licha ya kufanyika jitihada za misaada.

Shirika la madaktari wasio na mipaka limearifu kwamba maelfu ya watoto wanaendelea kukabiliwa na kitisho cha njaa na limeshutumu shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP kwa kuchelewa kuchukua hatua na kushindwa kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wa haraka.

Michango ya Dharura imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini Niger katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuonyeshwa na Vyombo vya habari duniani picha za watoto waliokondeana nchini humo.

Operesheni za kuwasidia watu milioni 3 na laki sita wanaokabiliwa na njaa hatimae zilianza kushika kasi lakini baada ya miezi kadhaa miito ya serikali iliambulia patupu.