1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Brazil zaonya dhidi ya matumizi ya nyuklia Ukraine

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

China na Brazil zimetoa wito dhidi ya matumizi au kitisho chochote cha silaha za nyuklia nchini Ukraine, katika hatua ya ukosoaji uliojificha kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

https://p.dw.com/p/4lBre
Rais wa China, Xi Jinping (kushoto) na Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva
Rais wa China, Xi Jinping (kushoto) na Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da SilvaPicha: Ken Ishii/Kyodo News/AFP

Kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa katika Umoja wa Mataifa ambayo pia ilitiwa saini na Afrika Kusini na Uturuki, mataifa hayo yametoa wito wa kujiepusha na matumizi au kitisho cha silaha za maangamizi makubwa, hususan silaha za nyuklia na za kibayalojia.

Mataifa hayo yanayoendelea kiuchumi yamesisitiza umuhimu wa suluhisho la amani kwa migogoro yote ya kimataifa.

Wiki hii Rais Putin alitishia kutumia silaha za nyuklia iwapo kutatokea shambulio kubwa katika ardhi ya Urusi. Huku Ukraine ikitaka kupewa silaha zaidi kutoka nchi za Magharibi ili kufanya mashambulizi katika ardhi ya Urusi.

Mataifa mengine yaliojiunga na wito huo wa Brazil na China ni pamoja na Algeria, Bolivia, Colombia, Misri, Indonesia, Kazakhstan, Kenya na Zambia.