1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jordan: Chama cha IAF chapata ushindi wa viti vya bunge

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Chama cha upinzani cha Kiislamu cha IAF nchini Jordan, ambacho ni tawi la chama cha Udugu wa Kiislamu, kimeshinda viti 31 kati ya 138 katika uchaguzi wa bunge.

https://p.dw.com/p/4kXb5
Jordan | Uchaguzi 2024 | Maafisa wakihesabu kura.
Maafisa wa uchaguzi Jordan wakiwa katika zoezi la kuhesabu kuraPicha: Jehad Shelbak/REUTERS

Licha ya chama hicho kuvishinda vyama vingine baada ya uchaguzi uliofanyika Jumanne, bado hakijafikia idadi inayotakiwa kuunda serikali.

Chama hicho kimekuwa kikitafuta kushika usukani kutokana na hasira iliyo miongoni mwa raia wa Jordan kuhusu mzozo Gaza.

Soa pia:Misri na Jordan zataka Isreal itekeleze azimio la Umoja wa Mataifa

Itakumbukwa kuwa nusu ya raia wa nchi hiyo wana asili ya Palestina. Akizungumza baada ya matokeo hayo Katibu Mkuu wa chama hicho Wael al-Saqqa amesema Gaza, Palestina na Jerusalem ni sehemu ya dira ya Jordan na watawatetea, kuhamasisha, na kuwasaidia watu wake wapate uhuru wao.