1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Israeli kuidhinisha rasmi serikali mpya ya Ehud Olmert

Dinah Gahamanyi4 Mei 2006

Ehud olmert anatarajiwa kuidhinishwa rasmi leo kama waziri mkuu mpya wa israel, na bunge la Israeli na hivyo kumuwezesha kuendelea na mpango wake wa kuchora upya mipaka ya israeli.

https://p.dw.com/p/CHLV
Ehud Olmert, kaimu waziri mkuu wa Israel
Ehud Olmert, kaimu waziri mkuu wa IsraelPicha: AP

Ehud Olmert aliyeteuliwa kama waziri mkuu wa muda wa israel, baada ya Ariol Sharon kuugua maradhi ya kiharusi mwezi Januari mwaka huu, atalitaka bunge la Israili kuidhinisha baraza la mawaziri 24 aliowachagua yeye baada ya chama chake cha mrengo wa kati cha kadima kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.

Katika kikao hicho kitakachoanza mchana , bwana Olmert anatarajiwa kubainisha sera muhimu za serikali yake, kabla kiongozi wa chama cha upinzani cha mrengo wa kulia cha Likud Benjamini Netanyahu kutoa hotuba yake.

Halafu wabunge watapiga kura kuidhinisha baraza jipya la mawaziri. Mgombea aliyependekezwa kiti cha spika wa bunge la Israeli kutoka chama cha kadima Dalia Yitzik, ataapishwa leo kama spika wa kwanza mwanamke kuliongoza bunge la israel.

Kikao hicho cha bunge kinachokaa leo, kimekuja baada ya kufanyika mazungumzo ya wiki nne baina ya chama cha kadima na vyama vingine 11 nchini Israeli, vilivyopata viti katika katika bunge la Palestina, kwa ajili ya kuunda muungano utakaoliwezesha taifa hilo kuondoa sehemu ya makazi yake katika eneo la West Bank.

Hata hivyo serikali mpya bado ina wingi zaidi wa viti bungeni, ikiwa na wabunge 67 kati ya viti 120, likiwajumuisha wabunge 29 kutoak achama cha kadima, 19 kutoka chama cha labour cha mlengo wa kati , na 12 kutoka chama cha othodox na 7 kutoka chama kinachopigania maslahi ya uzeeni.

Kwa upande mwingine Amil Perez kutoka chama cha Labour anayetarajiwa kuwa waziri wa ulinzi wa israel ameahidi kuimarisha usalama nchini humo amesema.

``Hatutakubali kwamba watoto wetu usiku na mchana wanalazimika kishi kwa woga. Kama walivyo watoto wetu wa wapalestina pia wanaishi kwa woga pia.

Kwa hiyo nitawambia wapalestina wabeba mustakabali wao mikononi mwao wenyewe na wafikirie uamuzi ambao utaepuka mapambano hayo yanayojiri hivi sasa. Nataka watu wote wajue kwamba sisi tuko tayari kutafuta suluhisho la amani, lakini hatuna nia hata kidogo kulegeza kamba mbele ya ughaidi.´´

Wakati huo huo rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema ameazimia kuwaomba wapalestina kupiga kura ya maoni juu ya mpango wowote wa amani na Israel. Hatua hiyo ya bwana abbas ni kinyume na sera ya serikali inayoongozwa na hamas nchini humo.

Akizungumza na gazeti la kila siku la Maariv nchini Israeli Abbas alisema Israel haipaswi kuacha kufufua mazungumzo ya mani na Palestina, licha ya kwamba Palestina inaongozwa na serikali ya Hamas.