Bundesliga hatimaye yaendelea na mechi zake baada ya maambukizi ya virusi vya corona kupungua Ujerumani, je, huu ndio mwanzo wa kandanda kurudi tena kote barani Ulaya? Vilabu vyote vya ligi kuu England vyaanza kuwapima wachezaji virusi vya corona kama sehemu ya maandalizi ya kurejea uwanjani na huko Kenya, je, kamati ya nidhamu ya Shirikisho la kandanda duniani FIFA litaipiga marufuku nchi hiyo?