1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOMU LAUA 5 ANGOLA

16 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFry

LUANDA: Watu 5 wamefariki ndani ya trekta moja na ndani ya traila pale bomu lililozikwa ardhini liliporipuka huko Angola ya Kati. Watu 3 waliofariki papo hapo na wengine 2 wakafa baadae hospitali.Magari hayo ambayo yalitolewa zawadi na jumuiya isio ya kiserikali ya Marekani-CARE INTERNATIONAL yaliteketea. Kiasi cha mabomu ya ardhini milioni 15 yalizikwa wakati wa vita vya kienyeji nchini Angola ambavyo vilimalizika mwaka jana.