1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobi Wine: Vikosi vya ulinzi vimezingira ofisi zetu za chama

22 Julai 2024

Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Bobi Wine amesema vikosi vya usalama vimeyazingira makao makuu ya chama chake leo Jumatatu ikiwa ni siku ya mkesha wa maandamano makubwa yaliyopangwa ya kupinga rushwa.

https://p.dw.com/p/4iaPy
Uganda Kampala | Polisi wakiwa nje ya chama cha NUP
Polisi wa Uganda wakiwa wameweka kambi nje ya ofisi za chama cha Bobi Wine cha National Unity Platform (NUP).Picha: SUMY SADURNI/AFP

Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Bobi Wine amesema vikosi vya usalama vimeyazingira makao makuu ya chama chake leo Jumatatu ikiwa ni siku ya mkesha wa maandamano makubwa yaliyopangwa ya kupinga rushwa na ambayo yamepigwa marufuku na mamlaka za nchi hiyo. 

Hatua ya kuzingizwa makao makuu ya chama cha Bobi Wine imekuja siku mbili baada ya rais Yoweri Museveni kuwaonya wanaopanga kushiriki kwenye maandamano hayo kesho Jumanne,kwamba wanacheza na moto. 

Soma pia:Waandamanaji Uganda waapa kuingia mitaani licha la onyo la Rais

Mwanasiasa wa upinzani anayeongoza chama cha NUP,Robert Kyagulani kwa jina maarufu Bobi Wine ameliambia shirika la habari la AFP kwamba makao makuu ya chama hicho yaliyoko kwenye mtaa wa Kavule mjini Kampala yamezingirwa na polisi na wanajeshi waliojihami kwa silaha. Raia wa Uganda wamepanga kuandamana hadi majengo ya bunge kesho.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW