BERLIN : Merkel amkaripia mshirika wake
13 Aprili 2007Kansela Angela Merkel wa Ujerumani leo hii amemkaripia mmojawapo ya washirika wake wa mikoa ambaye ni waziri mkuu wa mkoa wa Baden- Wuenttemberg Guenther Oettinger kwa kumsifu sana hakimu wa enzi ya utawala wa Manazi nchini Ujerumani.
Oettinger aliamsha hasira wiki hii kutokana na matamshi yake kwenye mazishi ya aliewahi kuwa waziri wa mkoa huo huo Hans Filbinger ambaye kugoma kujutia matendo yake wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Daunia kumekuwa kukileteya matatizo chama cha cha CDU.
Hadi kifo chake hapo April Mosi akiwa na umri wa miaka ya 93 Filbinger alikuwa akisisitiza kwamba ulikuwa ni wajibu wake akiwa kwenye jopo la mahakimu wa wanamaji kuwahukumu adhabu ya kifo mabaharia wanaolikacha jeshi.
Imeelezwa kwamba Merkel alimpigia simu Oettinger na kumwambia kwamba angelipendelea ziada ya kusifu mafanikio makubwa ya maisha ya Filbinger masuala mabaya kuhusu Manazi pia ingelipaswa kutajwa.
Oettinger aliwaambia waombolezaji kwamba Filbinger alikuwa sio Nazi bali mpizani wa utawala wa Manazi ambaye alikuwa hana chaguo bali kufanya kila analomriwa wakati wa utawala huo wa kidikteta.