Alizaliwa kama Abisai Marandu huko Moshi, kaskazini mwa Tanzania. Sasa anaishi kama Ab Mara, msanii wa muziki wa hip-hop katika mji wa Nürnberg ulio kusini mwa Ujerumani. Katika robo saa hii na Idhaa ya Kiswahili ya DW, mwanamuziki huyu anazungumzia ujumbe wa mapambano ya maisha kwenye muziki wake.