Mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa Idhaa ya kiswahili ya DW marehemu Isaac Muyenjwa Gamba, unasafirishwa leo asubuhi kwenda Mwanza, mji wa mwambao wa ziwa victoria uliopo kaskazini ya Tanzania ambapo kutakuwa na hafla fupi ya kuuaga kabla ya kupelekwa kijijini kwao katika wilayani Bunda mkoani Mara baadae mchana tayari kwa mazishi.