Waziri mkuu wa Uengereza bibi Theresa May amefungua njia ya kuitishwa mazungumzo yatakayodumu miaka isiyopungua miwili na ambayo mwisho wake itakuwa kutoka nchi hiyo ya kifalme katika Umoja wa ulaya// Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili ameuambia mkutano wa mataifa ya Kiarabu kwamba amani haiwezi kupatikana katika kanda hiyo bila kuanzishwa kwa taifa la Palestina karibu na Israel.