Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amekosoa kile alichokiita kuongezeka kwa sera za kuwabana wakimbizi barani Ulaya// Serikali ya Syria imeelezea wasiwasi juu ya habari kwamba wanajeshi 150 wa Marekani wameingia kaskazini mashariki mwa nchi hiyo// Shirika la ndege la Kenya - Kenya Airways linasema safari kumi za ndege zimefutwa leo kufuatia mgomo wa marubani.