Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ametoa wito wa kuchukuliwa hatua, kutoka kwa nchi, makampuni na watu wote kwa jumla kusaidia kufufua na kuhimiza upya mchakato wa haki za binadamu duniani kote// Mjini Mombasa mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yametangaza kuhuisha vuguvugu la pamoja kukabiliana na visa vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea kwenye kanda ya pwani nchini Kenya.