Mwanasheria wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Tundu Lisu ambaye ni Mkosoaji wa serikali ya Tanzania ametiwa mbaroni na polisi mchana wa leo// Mahakama Kuu nchini Uganda imewahukumu viongozi wanne wa Kiislam kifungo cha maisha gerezani// Serikali ya Afghanistan imeipongeza hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kutangaza kuwa atapekela wanajeshi zaidi nchini humo.