Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimetangaza kususia chaguzi zote za marudio za ubunge na madiwani zitakazofanyika kuanzia sasa kama hatua ya kupinga mwenendo wa uchaguzi wa mwishoni mwa wiki, kikisema ulitawaliwa na mizengwe ya wazi kwa lengo la kukipa ushindi chama tawala CCM.