Urusi- Sergei Ryabkov amesema kuwa Urusi inakaribia kuafikiana na Marekani kuhusiana na kusitishwa kwa vita katika mji wa Aleppo nchini Syria// Wakati Ujerumani inakamilisha mhula wake wa mwaka mmoja kama mwenyekiti wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya-OSCE, Waziri wake wa Mambo ya Nje, Frank-Walater Steinmeier, ameitolea wito Urusi kushirikiana kikamilifu.