1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa mauaji ya Shakahola Kenya waamriwa kutibiwa

Bruce Amani
21 Februari 2024

Mahakama ya Mombasa nchini Kenya imeamuru mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola Paul Mackenzie na wengine 94 kupelekwa hospitali mara moja baada ya washukiwa hao kuwasili mahakamani wakiwa wamedhoofika kiafya

https://p.dw.com/p/4cdYG
Mhubiri Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International
Mhubiri Paul Mackenzie na washukiwa wengine wanakabiliwa na mashitaka 238 ya kuuwa bila kukusudiaPicha: Halima Gongo/DW

Mahakama ya Mombasa nchini Kenya imeamuru mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola Paul Mackenzie na wengine 94 kupelekwa hospitali mara moja baada ya washukiwa hao kuwasili mahakamaniwakiwa wamedhoofika kiafya. Inasemekana washukiwa hao walikuwa wamesusia kula na kunywa maji kwa siku tatu.

Hakimu Mkuu Alex Ithuku alilazimika kwenda kuwaona washukiwa hao katika eneo la kuegesha magari la mahakama ya Mombasa waliposhindwa kutembea na wengine wasiweze hata kufungua macho. Upande wa mashtaka hata hivyo umepinga kukubaliwa kwa ombi lawashukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana.

Wamedai kuwa kwa sasa ni hatari washukiwa hao kuachiwa kwani haitakuwa rahisi kuwapata au kujua wanakoishi na pia wanahofia wanaweza kutoweka na kukwepa adhabu ya mashtaka yanayowakabili. Kesi hii itatajwa tarehe 5 Machi, mwaka huu wakati mahakama itakapopanga tarehe ya kutoa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka la kupinga dhamana.