1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinda amani wajeruhiwa katika mapigano mashariki mwa DRC

18 Machi 2024

Mapigano mapya yamezuka kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4dqDv
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bintou Keita
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bintou KeitaPicha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Askari wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Bintou Keita, amesema askari mmoja amejeruhiwa vibaya sana katika shambulio la mjini Sake lililotokea Jumamosi. Mji huo wa kimkakati upo kilometa 20 magharibi mwa Goma, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Watu walioshugudia wamesema mapigano yalizuka tena katika eneo hilo siku ya Jumamosi. Na kufikia mchana wa Jumapili, hali ya utulivu  ilikuwa imerejea katika mji huo.

Chanzo kimoja cha usalama kimeeleza kwa shirika la habari la AFP kwamba askari wa Umoja wa Mataifa walijeruhiwa, wakati mabomu mawili ya waasi wa M23 yalipotua kwenye kambi yao katika wilaya ya Mubambiro mjini Sake.

Kwa habari zetu zaidi tembelea chaneli yetu ya YouTube: