1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaazi Florida watahadharishwa juu ya kimbunga cha Idalia

30 Agosti 2023

Wakaazi wa jimbo la Florida nchini Marekani wanaoishi katika mazingira hatari ya pwani wameamriwa kuondoka kufuatia ripoti kuwa kimbunga Idalia kinaelekea eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4VjFG
Picha ya setilaiti ikionyesha sehemu ambazo huenda kimbunga Idalia kitazikumba
Picha ya setilaiti ikionyesha sehemu ambazo huenda kimbunga Idalia kitazikumbaPicha: NOAA/AP/picture alliance

Kimbunga hicho kinachoandamana na mvua kubwa na upepo mkali tayari kimepiga sehemu ya magharibi ya Cuba na kuiacha wilaya inayolima zao la tumbaku ya Pinar del Rio kwenye mafuriko huku wakaazi wengi wakikosa umeme.

Dhoruba hiyo inaripotiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 155 kwa saa na kutarajiwa kuelekea jimbo la Florida na viunga vyake.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Marekaniimetahadharisha kuwa, kimbunga hicho kina uwezo wa kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo ambalo bado lina makovu ya maumivu kufuatia kimbunga Ian kupiga eneo hilo mwaka uliopita.

Kimbunga Idalia itakuwa dhoruba ya kwanza kuikumba Florida katika msimu huu wa vimbunga, japo ni muendelezo wa matukio ya hivi karibuni ya majanga ya asili ikiwemo moto wa nyika katika kisiwa cha Hawaii, Canada na Ugiriki.