1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yamzuia balozi wa Marekani kumtembelea mwandishi

27 Aprili 2023

Urusi imesema haitamruhusu balozi wa Marekani kumtembelea mwandishi wa habari wa Marekani aliyezuiliwa nchini humo Evan Gershkovich

https://p.dw.com/p/4Qddr
Russland | WSJ Reporter Evan Gershkovich vor Gericht in Moskau
Picha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov mwishoni mwa wiki iliyopita alilalamikia Marekani kwa kukataa kuwapa visa waandishi wa Urusi waliotarajiwa kwenda naye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Taarifa ya wizara hiyo imesema uuamuzi huo unafuatia kile ilichokitaja kama uamuzi wa kichokozi wa Marekani na kuonya juu ya hatua nyingine za kisasi ambazo bado zinaandaliwa.

Gershkovich alikamatwa nchini Urusi mwezi uliopita, kwa madai ya kufanya ujasusi.