1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Urusi na China zapinga rasimu ya azimio la Marekani

23 Machi 2024

Urusi na China zimetumia kura zao za turufu kuipinga rasimu ya azimio lililopendekezwa na Marekani la usitishaji mapigano katika ukanda wa Gaza. Algeria pia imepiga kura ya kupinga azimio hilo wakati Guyana ikijizuia.

https://p.dw.com/p/4e36N
Ukraine-Krise der chinesische Botschafter in den USA Zhang Jun bei einer Krisensitzung des UN-Sicherheitsrats
Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang JunPicha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

China na Urusi pamoja na mataifa mengine ya Kiarabu yamesema lugha iliyotumika kwenye rasimu hiyo ni dhaifu mno na kamwe hailengi kuiwekea Israel shinikizo lolote.

Licha ya pingamizi la Urusi na China, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema wanadiplomasia wataendelea na juhudi za kutafuta mwafaka juu ya maandishi sahihi yanayokubalika na kila upande kwenye rasimu hiyo ya azimio.

Soma pia: Mashambulizi ya Israel katika hospitali ya al-Shifa yaua watu 140

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzia amesema kwa jinsi maandishi yalivyo kwenye rasimu hiyo, itafungua mlango kwa Israel kuendelea kuvunja sheria bila ya kujali.

Mwanadiplomasia wa Marekani Antony Blinken amezishtumu China na Urusi kwa kutumia nguzu zao za kura ya turufu kwa maslahi yao binafsi huku kundi la Hamas likikaribisha uamuzi uliochukuliwa na Beijing na Moscow.