1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi kwenye hatua za mwisho kujiondowa Mkataba wa Nyuklia

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Wabunge wa Urusi wamepiga kura leo kubatilisha hatua ya serikali ya nchi hiyo kuridhia Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio na Matumizi ya Silaha za Nyuklia (INF).

https://p.dw.com/p/4XdhY

Hii ni hatua ya mwisho mwisho kukaribia kwenye kilele cha kuachana na makubaliano hayo ya kihistoria yanayopiga marufuku kufanyia majaribio silaha hizo.

Urusi na Marekani ziliusaini mkataba huo mnamo 1996, lakini Marekani haijawahi kuyaridhia rasmi makubaliano hayo.

Soma zaidi: Hofu yazidi kuhusu Urusi kujitowa katika mkataba wa INF

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais Vladimir Putin wa Urusi kusema mwanzoni wa mwezi huu kwamba hakuwa tayari kusema ikiwa Urusi ilihitaji kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

Matokeo ya bunge la Urusi, Duma, yameonyesha wabunge wameridhia kwa kauli moja muswada uliowasilishwa na kusomwa kwa mara ya kwanza bungeni.