1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Upinzani Togo waitisha maandamano dhidi ya Rais Gnassingbe

28 Machi 2024

Wanaharakati na viongozi wa upinzani katika taifa la Togo huko Afrika Magharibi wamewataka raia wa nchi hiyo waandamane ili kumzuia rais kusaini katiba mpya itakayofutilia mbali uchaguzi wa miaka ijayo nchini humo.

https://p.dw.com/p/4eDRM

Wanaharakati na viongozi wa upinzani katika taifa la Togo huko Afrika Magharibi wamewataka raia wa nchi hiyo waandamane ili kumzuia rais kusaini katiba mpya itakayofutilia mbali uchaguzi wa miaka ijayo nchini humo na kurefusha utawala wake wa miongo kadhaa hadi mwaka 2031.

Katiba hiyo iliyopitishwa na wabunge nchini humo mapema wiki hii ila ambayo kwa sasa inasubiri idhini ya mwisho ya Rais Faure Gnassingbe, inalipa bunge nguvu za kumchagua rais na kuondoa kabisa nguvu ya wananchi kumchagua kiongozi wao wa nchi. Hatua hii, inamsafishia njia Gnassingbe kuchaguliwa tena, muhula wake utakapofika mwisho mwakani.

Soma pia: Togo: Wabunge sasa kumchagua Rais katika katiba mpya

Baadhi ya wataalam wa kisheria wanasema, katiba hiyo inayabinya mamlaka ya marais wajao katika nchi hiyo, kwa kuwa sasa rais atakuwa anaongoza kwa muhula mmoja huku nguvu kubwa ya uongozi ikiwa kwa mtu ambaye atakuwa kama waziri mkuu.