1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wasyria wanaorejea nyumbani wanakabiliwa na unyanyasaji

13 Februari 2024

Ripoti mpya iliyochapishwa Jumanne na Umoja wa Mataifa inasema raia wa Syria wanaorejea kwenye taifa hilo lililoharibiwa kwa vita wanaandamwa na ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo mateso na unyanyasaji wa kijinsia.

https://p.dw.com/p/4cM3b
Wasyria wakiandamana mjini Koblenz, Ujerumani
Waandamanaji wa Syria UjerumaniPicha: Bernd Lauter/Getty Images/AFP

Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imekusanya ushuhuda wa Wasyria waliorejea nyumbani ambao wametoa taswira ya hali ya kutisha wanayokabiliana nayo kwenye nchi hiyo.

Imekusanya simulizi za unyanyasaji na mateso ikiwemo watu kukamatwa bila makosa na kudhulumiwa kingono, vitendo ambavyo vinatuhumiwa kufanywa na maafisa wa serikali ya Syria.

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema taswira halisi ya hali nchini Syria imetolewa kupitia ripoti hiyo katika wakati idadi ya Wasyria wanaolazimishwa kurejea nchini mwao kutoka mataifa mengine inaongezeka.

Syria ilitumbukia vitani tangu mwaka 2011 kufuatia maandamano ya umma ya kutaka kuung'oa utawala wa rais Bashar al-Assad bila mafanikio.