1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ulaya yahimiza kasi zaidi ya misaada kwa Ukraine

Lilian Mtono
15 Machi 2024

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel ameonya jana kwamba mustakabali wa vita vya Ukraine huenda ukajulikana katika miezi ijayo na kuwahimiza washirika kuongeza kasi ya kupeleka misaada nchini humo.

https://p.dw.com/p/4dXMK
Mkutano wa wafadhili wa Umoja wa Ulaya kwa Syria
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel ameendelea kuwahimiza washirika wao kuisaidia haraka UkrainePicha: Geert Vanden Wijngaert/AP/dpa/picture alliance

Borrel amewaambia waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Washington kwamba amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake yote juu ya athari kwa Ukraine ikiwa Urusi itashinda vita hivyo.

Amesema, kama Rais Vladimir Putin atashinda na kuweka vibaraka wake kama alivyofanya nchini Belarus, ni wazi kuwa harakati zake hazitaishia hapo na kutaka misaada kupelekwa haraka.

Akiwa nchini humo, Borrel amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken