1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yataka uchunguzi wa kimataifa kuhusu ajali ya ndege

Tatu Karema
25 Januari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa wito wa uchunguzi wa kimataifa kuhusu ajali ya ndege ya jeshi la Urusi iliyotokea Jumatano katika eneo la mpaka wa Belgorod Magharibi mwa Urusi

https://p.dw.com/p/4be5p
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky awasili katika mkutano wa kilele huko Granada Kusini mwa Uhispania mnamo Oktoba 5, 2023
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Thomas Coex/AFP

Katika hotuba yake ya jana jioni, Zelensky amesema kuwa huduma ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine HUR, kwasasa, inajaribu kuchunguza zaidi kuhusu hatima ya wafungwa wa kivita wa nchi hiyo ambao kulingana na Urusi walikuwa ndani ya ndege hiyo.

Soma pia: Wafungwa 65 wa kivita wafa baada ya ndege ya Urusi kuanguka

Zelensky pia amemuagiza waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Dmytro Kuleba kutoa habari zote zinazojulikana na Ukraine kwa washirika wa kimataifa.

Kulingana na ripoti zaUrusi, ndege hiyo ya kijeshi aina ya Ilyushin chapa II-76 ilikuwa na abiria 74 ambao wote wamefariki.

Hata hivyo, hakuna habari huru kuhusu nani ama nini kilichobebwa ndani ya ndege hiyo.