1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi athibitisha uchaguzi utafanyika 2023 nchini Congo

Jean Noël Ba-Mweze
12 Desemba 2022

Katika hotuba yake mbele ya Bunge la Kitaifa pamoja na Seneti ,Tshisekedi alibainisha kuwa shughuli za kuwatambua na kuwasajili wapigakura zitaanza tarehe 24 Desemba.

https://p.dw.com/p/4Kphu
Rais Tshisekedia aahidi kuweko na uchaguzi huru
Rais Tshisekedia aahidi kuweko na uchaguzi huru Picha: Giscard Kusema/Presse- und Kommunikationsdienst der Präsidentschaft von Kongo

Rais Félix Tshisekedi alisisitiza kwamba uchaguzi  utagharamiwa kwa ujumla na Serikali ya Kongo. Na hivyo kawaalika Wakongo wanaoruhusiwa kisheria kujisajilisha ili kupiga kura. Yaani mambo yote yako  tayari ili kuanzisha operesheni ya kuwasajili wapiga kura, kama alivyohakikisha Sylvie Birembano, mmoja wa viongozi wa tume huru ya uchaguzi hapa nchini CENI.

"Tume huru ya uchaguzi tayari imeanza kipindi cha kurekebisha orodha ya uchaguzi kupitia operesheni ya kuwatambua na kuwasajili wapiga kura. Tayari tumepokea vifaa vya kusajilisha kutokea kwa mshirika wetu Nero system na hivyo tunawahimiza wananchi kushiriki operesheni hiyo kuu."

''Ni muhimu kujisajilisha''

Jambo linaloungwa mkono na baadhi ya Wakongo hususan wale walio upande wa vyama vilivyo madarakani. Daddy Bijafu ni mmoja wa wale Wakongo wanaoamini uchaguzi utafanyika December 20 mwaka 2023 kama ilivyopangwa, anaomba pia wananchi wengine kujiandikisha kupiga kura.

"Tunapaswa kuunga mkono tume huru ya uchaguzi tukijiandikisha kwa uwingi kwani huu sasa ni mwanzo wa operesheni ya kuwasajili wapiga kura. Ni vema raia kuhimizwa ili kuelewa kwamba madaraka ni yao. Halafu ili uchaguzi kufanyika ipasavyo na matakwa ya wanainchi kutekelezwa, ni muhimu kujisajilisha." 

Wasiwasi wa mashirika ya kiraia

Changamoto za maandalizi ya uchaguzi bado ni nyingi
Changamoto za maandalizi ya uchaguzi bado ni nyingiPicha: picture-alliance/dpa

Lakini bado wapo wengi Wakongo ambao hawajaamini uchaguzi utafanyika tarehe 20 decemba 2023 kwani muda umebaki kidogo ili kuukamilisha mchakato, hususan mda wa kuwahesabu wapiga kura. Wataalam wa mashirika ya kiraia wana mashaka kabisa pamoja na wasiwasi kuwa labda washindi tayari wameandaliwa, kama anavyoeleza Dieudonné Mushagalusa, mratibu wa wataalam wa mashirika za kiraia.

"Uchaguzi hautafanyika kwani ukifuatana na namna inabidi kufanya uchaguzi halali, uchaguzi ambao unaoweza kuleta matokeo watu wanayoyahitaji hautafanyika wakati huo. Wakisema watafanya uchaguzi ni kusema wamekwishajua yule ambae atashinda uchaguzi huo kwani wakati ambao wanatayarisha kufanya hesabu ya watu ambao watapiga kura haiwezekani katika inchi ya Kongo."

Wakati hayo yakijiri, upinzani unaendelea kudai kuwe na makubaliano baina ya tume huru ya uchaguzi na wote watakaoshiriki mchakato huo.