1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Serikali yaondoa uwezekano wa kurudiwa kwa uchaguzi

28 Desemba 2023

Msemaji wa serikali ya Kongo Patrick Muyaya amesema matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita hayatafutwa licha ya miito inayojirudia kutoka kwa wagombea wa upinzani kutaka uchaguzi wote urudiwe.

https://p.dw.com/p/4afdl
DR Kongo, Kinshasa | Maandamano ya kupinga uchaguzi
Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Martin Fayulu wakipiga kambi mbele ya makao makuu ya chama chake mjini KinshasaPicha: JOHN WESSELS/AFP

Matokeo ya uchaguzi huo wa Desemba 20 yanaonyesha kuwa Rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi anaongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya wapinzani wake.

Hali ya mvutano unaozidi kuhusiana na uchaguzi huo inatishia kuivuruga zaidi Kongo, ambayo tayari inapambana na mzozo wa usalama katika maeneo ya mashariki.

Hapo jana polisi mjini Kinshasa ilivunja maandamano ya watu wanaopinga namna uchaguzi wa rais na bunge ulivyoendeshwa.

Upinzani unasema uchaguzi huo ulikumbwa na kasoro nyingi na udanganyifu, madai ambayo tume ya uchaguzi, CENI inayakanusha.

Muyaya amesema wapinzani wanapaswa kusubiri hadi matokeo kamili yatangazwe ndiyo wayapinge katika mahakama ikiwa hilo litahitajika.