1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Muda wa Ujerumani kuwa na rais mwanamke umefika

14 Mei 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameonesha kuamini kwamba,muda umefika kwa Ujerumani kuwa na rais mwanamke.

https://p.dw.com/p/4fqDH
Baltische Regierungschefs treffen sich zu Pressekonferenz in Riga
Picha: Gints Ivuskans/AFP

Katika mahojiano na gazeti la habari la Stern la nchini Ujerumani Kansela Scholz amesema angefurahi ikiwa atachaguliwa mwanamke katika nafasi ya rais mnamo mwaka 2027 ambayo hivi sasa inashikiliwa na Frank-Walter Steinmeier.

Tangu mwaka 1949 Ujerumani imeshakuwa na marais 12 wanaoongoza serikali ya shirikisho na wote wamekuwa wanaume.

Angela Merkel aliyeiongoza Ujerumani mwaka 2005 hadi 2021 ni mwanamke pekee aliyewahi kushikilia nafasi  ya Ukansela tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya shirikisho la Ujerumani.