1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa BRICS wajadili kuongeza wanachama wapya

Bruce Amani
23 Agosti 2023

Mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoendelea kwa kasi duniani la BRICS, leo umeingia siku ya pili itakayotawaliwa na mjadala muhimu wa kutanua ukubwa wa kundi hilo.

https://p.dw.com/p/4VTbm
Mkutano wa 15 wa BRICS Afrika Kusini
Viongozi wa mataifa yanayounda kundi la BRICS, Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.Picha: BRICS/Handout/AA/picture alliance

Mkutano wa kilele wa kundi la mataifa yanayoendelea kwa kasi duniani la BRICS, leo umeingia siku ya pili itakayotawaliwa na mjadala muhimu wa kutanua ukubwa wa kundi hilo kwa kuyakaribisha mataifa mengine kuwa wanachama.

Katika siku ya kwanza ya mkutano huo unaofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, viongozi wa mataifa hayo ya Brazil, China, India, Afrika Kusini na Urusi, walitoa hotuba zilizomulika mwelekeo wa kundi hilo la kiuchumi na nafasi yake katika ulimwengu wa sasa. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alielezea matarajio yake.

Soma pia: Ni kwa nini Saudia na nchi nyingine zataka uanachama BRICS?

Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye alihutubia jukwaa hilo kwa njia ya mtandao, alisema kundi hilo limepiga hatua katika utekelezaji wa dhamira yake ya kuachana na utegemezi wa dola ya Marekani katika biashara na uchumi.

Hotuba za viongozi wengine ikiwemo rais Xi Jinping wa China, ziligusia umuhimu wa kuimarisha nafasi ya kundi la BRICS kwenye Jukwaa la Kimataifa. Mataifa ya BRICS yanawakilisha robo ya uchumi wa ulimwengu.