1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Mikutano ya Papa Francis yaahirishwa baada ya kuugua mafua

25 Novemba 2023

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameahirisha mikutano yake yote iliyokuwa imepangwa leo hii kutokana na ugonjwa wa mafua.

https://p.dw.com/p/4ZREA
Vatikanstadt 2023 | Papst Franziskus bei der wöchentlichen Generalaudienz
Papa FrancisPicha: Riccardo De Luca/UPDATE IMAGES PRESS/MAXPPP/dpa/picture alliance

Taarifa hii iliyotolewa na Vatican inajiri wiki moja kabla ya safari ya  Papa Francis  kuelekea Dubai ambapo atashiriki Desemba 2 mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya Hewa wa COP28, ambako anatarajiwa kukemea ukosefu wa hatua na kuhimiza kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira.

Afya ya Papa Francis imekuwa ikidhoofika katika miezi ya hivi karibuni, na kumlazimu kutumia kiti cha magurudumu na hivyo kuzusha uvumi wa kujiuzulu kwake, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Papa Benedict wa XVI.