Miaka 46 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
26 Aprili 2010Matangazo
Kuzaliwa kwa Tanzania kulijiri katika wakati wa kusisimua wa kumalizika ukoloni katika nchi nyingi za Afrika na kuchomoza hisia za kutaka Umoja wa Bara zima la Afrika, na hata Afrika nzima iwe na serikali moja.
Mmoja kati ya mashahidi wa kuzaliwa Muungano wa Tanzania ni Hassan Nassor Moyo, aliyekuwemo katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi yaliofanyika miezi mitatu tu kabla ya kuundwa Muungano huo; na pia akatumikia serikali ya Muungano baadae.
Othman Miraji alizungumza naye na kumuuliza kwanza kile kilichowachochea watu waliouasisi Muungano huo, marehemu marais wa Tanganyika na wa Zanzibar, Julius Nyerere na Abedi Karume, kuja na wazo hilo...
Mtayarishi: Othman Miraji
Mpitiaji: Mohamed Abdulrahman