1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Marekani yazima shambulizi ya Wahouthi huko Bahari ya Shamu

27 Desemba 2023

Marekani imesema imedungua ndege 12 zisizo na rubani pamoja na makombora 5 yaliyofyetuliwa na waasi wa Houthi wa nchini Yemen kusini mwa Bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4abF2
Meli ya mizigo ikikatisha Bahari ya Shamu
Mashambulizi ya waasi wa Houthi wa Yemen yanayozilenga meli za mizigo yameongezeka kwenye Bahari Nyekundu tangu kuanza kwa vita vya Ukanda wa Gaza.Picha: Sayed Hassan/dpa

Kamandi ya Jeshi la Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati imetoa taarifa hizo kupitia mtandao wa kijamii wa X ikisema kwenye makabiliano hayo hakuna meli iliyoharibiwa wala majeruhi au kifo kilichotokea.

Kabla ya taarifa hiyo waasi wa Houthi walisema wameishambulia meli moja ya mizigo baada ya manahodha wake kukaidi tahadhari zilizotolewa. Kampuni inayomiliki meli hiyo ya MSC United ilithibitisha kulengwa na hujuma za Wahouthi lakini wafanyakazi wake wote wako salama.

Tangu kuzuka kwa vita kwenye Ukanda wa Gaza, waasi wa Houthi wamekuwa wakizilinga meli nyingi za mizigo zinazokatisha Bahari Nyekundu kushinikiza kukomeshwa kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza.