1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yaanza kuondoa wanajeshi wake nchini Niger

19 Mei 2024

Marekani imeanza kuondoa wanajeshi wake kutoka Niger baada ya kuombwa kufanya hivyo na watawala wa kijeshi wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4g3KR
Sehemu ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Niger
Sehemu ya wanajeshi wa Marekani waliopo nchini Niger Picha: Alex Fox Echols Iii/Planetpix/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Tangazo la kuanza kuondoka wanajeshi hao limetolewa kwa pamoja na nchi hizo mbili mapema hii leo.

Taarifa hiyo imesema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kabla ya Septemba 15. Pande hizo zilitangaza kufikia makubaliano ya kuondolewa wanajeshi hao waliopelekwa kuisaidia Niger kupambana na makundi ya itikadi kali za dini.

Utawala mpya wa kijeshi ulioipindua serikali ya kidemokrasia katikati mwa mwaka jana ulisema wanajeshi hao wa Marekani walikuwemo nchini Niger kinyume cha sheria.

Kwa jumla Marekani inao askari 650 nchini Niger pamoja na kambi kubwa ya droni karibu na mji wa kaskazini mwa taifa hilo wa Agadez.