1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Watu 1,500 wafa Haiti kutokana na vurugu za kihalifu

28 Machi 2024

Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linasema uhalifu wa magenge nchini Haiti umesababisha vifo vya watu 1,500 mwaka huu

https://p.dw.com/p/4eEHv
Haiti yakumbwa na machafuko
Mmoja ya watu wanaounda genge la G9 and Family akiviringisha tairi kwa ajili ya kulichoma kwenye kizuizi cha barabarani katika kitongoji cha Delmas 6 cha Port-au-Prince, Haiti, Machi 11, 2024.Picha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Kulingana na ripoti hiyo mamia ya watu walichomwa moto na magenge yanayodai kwamba yalikuwa yanajilinda.

Katika taarifa iliyotolewa leo pamoja na ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na hali ya taifa hilo la Karibia, mkuu wa shirika hilo Volker Turk ametoa wito wa vitendo hivyo kukomeshwa mara moja.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu 4,451 waliuwawa mwaka jana huku hao zaidi ya 1,500 wakiwa wamefariki dunia kufikia Machi 22 huku machafuko yakizidi.

Machafuko ya Haiti yameshuhudia magenge yaliyojihami kuvamia vituo vya polisi na uwanja wa ndege wa kimataifa nchini humo. Waziri Mkuu Ariel Henry, alitangaza kujiuzulu mnamo Machi 11.