1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wadhibiti eneo jingine mashariki mwa DRC

8 Machi 2024

Waasi wa M23 wamedhibiti eneo jingine, wakati mapigano yakiendelea kwa siku ya tatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Maelfu ya raia wanaendelea kukimbia mapigano wakitafuta usalama.

https://p.dw.com/p/4dJQM
Waasi wa kundi la M23  nchini DRC
Waasi wa M23 wakiwa katika harakati zao mjini Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/File/picture alliance

Duru zinasema kufikia jana Alhamis, M23 walikuwa wameudhibiti mji wa Kibirizi, ulioko kilometa karibu 30 upande wa Kaskazini Mashariki. Afisa mmoja wa utawala katika eneo hilo alilieleza shirika la habari la AFP kwamba, M23 walidhibiti mji huo baada ya kufyatuliana risasi na wanajeshi wa Kongo na wapiganaji wanaoiungamkono serikali. Mkazi mwingine Gervais Kambale kutoka eneo la karibu la Kanyayonga ambalo raia wanaokimbia wamekuwa wakiwasili kwa wiki nzima, amesema wameshuhudia mamia ya watu waliokuwa njiani kuelekea upande wa kaskazini. Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 100,000 wamekosa makaazi wiki hii, wengi ni kutoka mji wa Nyanzale wa Kivu Kaskazini.