1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiwango cha ukosefu wa ajira Afrika Kusini chaongezeka

15 Mei 2024

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Afrika Kusini kimeongezeka katika robo ya kwanza ya mwaka huu na kuiacha serikali ikiwa na wasiwasi wiki chache tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/4frH3
Mwandamanaji akiwa ameshikilia bango wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Uhuru mjini Pretoria
Mwandamanaji akiwa ameshikilia bango wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Uhuru mjini PretoriaPicha: Themba Hadebe/AP/dpa/picture alliance

Ofisi ya taifa ya takwimu imesema kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia asilimia 32.9 kati ya mwezi Januari na Machi, ongezeko hilo likiwa asilimia 0.8 tofauti ya kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Ofisi hiyo ya takwimu imeendelea kueleza kuwa, idadi ya watu wasiokuwa na ajira iliongezeka kwa 330,000 hadi milioni 8.2.

Soma pia: Afrika Kusini yaadhimisha miaka 30 ya demokrasia

Ukosefu wa ajira ni moja kati ya masuala muhimu ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu Mei 29. Vijana wengi wanalalamikia ukosefu wa ajira katika taifa ambalo linachukuliwa kuwa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Uungwaji mkono kwa chama tawala cha African National Congress (ANC), kilichokuwa madarakani tangu mwaka 1994, umepungua hadi chini ya asilimia 50 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika.