1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa magenge Haiti aapa kuendelea na mapambano

14 Machi 2024

Kiongozi wa magenge mwenye nguvu Haiti Jimmy Cherizier, ameapa kuendelea na mapigano yaliyoitumbukiza nchi hiyo katika machafuko, wakati washikadau wakijaribu kuunda usimamizi wa mpito utakaochukua nafasi ya Ariel Henry.

https://p.dw.com/p/4dW2b
Jimmy "Barbecue" Cherizier
Kiongozi wa magenge mwenye nguvu Haiti Jimmy CherizierPicha: REUTERS

Cherizierambaye kwa jina la utani anaitwa "Barbecue" kupitia redio inayotangaza kwa lugha ya Kihispania ya W Radio, amesema muungano wake wa makundi yaliyojihami, haujali kuhusiana na kujiuzulu kwa Henry na kwamba wataendelea kupigania uhuru wa Haiti.

Cherizier ni afisa wa zamani wa polisi ambaye amewekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.

Mataifa yaanza kuwaondoa raia wao Haiti

Haiti haijafanya uchaguzi tangu mwaka 2016 na kwa sasa hakuna rais wala bunge. Hakukuchaguliwa mtu atakayemrithi rais Jovenel Moise ambaye aliuwawa mwaka 2021 huku Henry akiiongoza nchi hiyo baada ya kifo chake.