1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAzerbaijan

Kiongozi wa Azerbaijan kutohudhuria mazungumzo ya Karabakh

4 Oktoba 2023

Rais wa Azerbaijan hatohudhuria mazungumzo juu ya mzozo wa jimbo la Nagorno-Karabakh yaliyopangwa kufanyika pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya unaoanza kesho huko Granada nchini Uhispania.

https://p.dw.com/p/4X7Xr
Maandamano ya Warmenia wanaoishi mjini Brussels
Maandamano ya Warmenia wanaoishi mjini BrusselsPicha: Nicolas Landemard/Le Pictorium/IMAGO

Shirika la Habari la nchi hiyo limeripoti kwamba rais Ilham Aliyev hatoshiriki mkutano huo uliotayarishwa kesho kwa kile kimetajwa kuwa "mitazamo ya kuipinga Azerbaijan" miongoni mwa washiriki wengine walioalikwa.

Kulikuwa na matumaini kwamba mkutano wa Granada utatoa nafasi kwa Aliyev kukutana na kiongozi mwenzake wa Armenia Nikol Pashinyan na kusawazisha mahusiano yao yaliyotiwa doa na mzozo wa kuwania jimbo la Karabakh.

Mwishoni mwa mwezi Septemba jeshi la Azerbaijan lilichukua udhibiti kamili wa jimbo hilo baada ya siku mbili za mapigano makali na makundi ya Waarmenia waliokuwa wanataka kujitenga kwa jimbo la Karabakh.